Dhana ya mofimu

Hamjambo wasomaji wapendwa? Karibuni katika kipindi cha leo. Nimejitayarisha vizuri kueleza dhana ya mofimu katika lugha ya Kiswahili. Mofimu ni nini? Mofimu ni kipashio kidogo katika lugha ambacho hakiwezi kugawika zaidi bila kupoteza maana yake ya kisarufi. Ikumbukwe kuwa kiambishi ni mofimu ambayo huongezwa kabla au baada ya mzizi wa neno ili kuwakilisha dhana fulani….

Jedwali la Konsonanti za Kiswahili

Jedwali lifuatalo ni muhimu sana katika kuelezea uainishaji wa konsonanti za Kiswahili. Kutokana na jedwali hili tunaweza kutambua mambo yafuatayo; Mahali konsonanti hutamkiwa. Ni ghuna au sighuna Namna hewa inavyobanwa. Kumekuwa na mjadala kuhusu sauti /j/. Je,ni kipasuo au kipasuo-kwamizwa? Swali hili litajibiwa katika makalo yatakayofuata.   H- hafifu/sighuna Gh- ghuna